'Vifo vyatokea' kwa kutotilia maanani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Somalia

Maelfu ya vifo ambavyo vingeweza kuzuilika vilitokea kutokana na baa la njaa Afrika Mashariki mwaka jana kwasababu jumuiya za kimataifa zilishindwa kutilia maanani onyo la awali, yamesema mashirika mawili ya kutoa misaada ya Uingereza.

Oxfam na Save the Children yamesema yamechukua zaidi ya miezi sita kwa mashirika ya kutoa misaada kufanyia kazi onyo lililotolewa kuhusu kutokea kwa baa hilo la njaa.

Kati ya watu 50,000 and 100,000 wamefariki dunia Kenya, Ethiopia na Somalia.

Mashirika hayo yamesema serikali, wafadhili, Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanahitaji kujifunza kutokana na makosa yaliyofanyika.

Katika ripoti yenye kichwa cha habari A Dangerous Delay, mashirika yamesema utamaduni wao wa kuwa na wasiwasi juu ya hatari watakazokumbana nazo ndizo zilizozuia jitihada kubwa ya kutoa misaada.

Wamesema sehemu ya tatizo hilo ni serikali za Kenya na Ethiopia kutokukiri ukubwa wa tatizo hilo, lakini pia wafanyakazi wa shirika hilo la kutoa msaada walihisi wameshawahi kushuhudia mara nyingi tatizo hilo.

Ripoti hiyo ilisema, "Wafadhili wengi walikuwa wanataka ushahidi wa kuwepo maangamizi yaliyowakumba binadamu kabla ya kuzuia balaa lisitokee."

"Mifumo ya kisasa ya kutoa onyo mapema, mwanzo ilitoa uwezekano wa kuwepo dharura mapema mwezi Agosti 2010, lakini utekelezaji wa kuokoa suala suala hilo halikufanyika mpaka Julai 2011."

Mpaka kufikia wakati huo "idadi ya watu wenye utapiamlo katika baadhi ya maeneo Afrika Mashariki yalishazidi kiwango cha kuitwa dharura na tayari vyombo mbalimbali vya habari vilianza kuzungumzia baa hilo la njaa".