Huwezi kusikiliza tena

Uhuru Kenyatta azungumza

Mahakama ya kimataifa ya ICC inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu ikiwa washukiwa wakuu sita wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2007 wana kesi ya kujibu siku ya Jumatatu.

Kuelekea mwishoni mwa mwaka uliopita, majaji katika ICC walisikiliza upande wa mashtaka na pia utetezi kutathmini ikiwa kuna ushahidi wa kutosha wa kuwashtaki washukiwa hao.

Miongoni mwa washukiwa hao ni naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta , na waziri wa zamani William Ruto, ambao wanadhamiria kugombea kiti cha Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Mwandishi wetu aliyopo Nairobi Anne Mawathe amezungumza na Bw Kenyatta kwanza kufahamu hisia zake binafsi hasa katika maisha yake ya kifamilia.