Marekani yakerwa 'kukojolewa' kwa maiti

Huwezi kusikiliza tena

Waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta amesema video inayoonyesha askari wa jeshi la majini la Marekani wakikojolea maiti za Wafghanistan ni la "kusikitisha sana".

Alisema, wale walioshiriki katika tukio hilo kwa namna moja au nyingine watachukuliwa hatua "kali sana".

Video hiyo, iliyowekwa kwenye mtandao, imekusudia kuonyesha wanajeshi wanne wa majini wakiwa wamesimama juu ya miili ya wapiganaji hao wa kitaliban, ambapo japo mmoja alikuwa amejaa damu.

Chanzo cha video hiyo hakijajulikana.

Bw Panetta amemwamuru kamanda wa Marekani na majeshi ya Nato nchini Afghanistan, Jenerali John Allen, kuchunguza suala hilo.

Katika taarifa yake, Bw Panetta alisema aliona video hiyo.

"Tabia hii kwa hakika inasikitisha sana. Tabia hii haikubaliki kabisa kwa wote walio kwenye jeshi la Marekani."

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Pentagon imesema inachunguza uhalisia wa video hiyo, lakini hakuna lolote kuashiria kuwa video hiyo si halisi.

Bw Panetta hakukana uhalisia wa video hiyo.