Iran yajaribu kombora jipya

Iran inasema imefanya jaribio la kurusha kombora la masafa ya wastani.

Jaribio hilo lilifanywa wakati wa mazoezi ya jeshi karibu na Hormuz, mlango unaounganisha Ghuba na Bahari ya Hindi.

Jeshi la wanamaji la Iran linasema siku ya mwisho ya mazoezi Jumatatu, meli zitaweza kupita kwenye njia ya Hormuz, ikiwa tu jeshi hilo litaziruhusu. Mkondo wa Hormuz ni njia inayopitwa na meli nyingi zinazobeba mafuta, na Iran inatishia kuifunga endapo itawekewa vikwazo zaidi.