Nigeria yataka zidisha bei ya mafuta

Wakuu wa Nigeria wametangaza mpango kuhusu mafuta utaozusha malalamiko - mpango wa kuacha kufidia bei ya mafuta.

Haki miliki ya picha AFP

Fidia hiyo inayogharimu serikali dola bilioni 8 kila mwaka, inapunguza bei ya mafuta, na ikiondoshwa mafuta yatapanda sana.

Mipango kama hiyo imepingwa vikali na vyama vya wafanyakazi wa Nigeria.

Watu wengi wanaona bei nafuu ya mafuta ndiyo manufaa pekee wanayopata kutoka utajiri wa mafuta wa taifa.