Wanasiasa walaumiwa kwa mauwaji

Mamiya ya watu wameuawa kwa visu na mapanga baada ya kukimbia mapigano ya kikabila huko kusini mwa Sudan, kwa mujibu wa duru mbalimbali.

Mjumbe wa tume ya maridhiano na amani, John Boloch amesema takriban watu 150 wengi wao wanawake na watoto wameuawa katika siku mbili zilizopita.

Mwanamke mwingine ameiambia BBC kua watu 20 kutoka familia yake waliuawa kwa kupigwa risasi.

Wapiganaji wapatao 6,000 kutoka kabila la Lou Nuer wamekua wakiwafuata watu wa kabila la Murle.

Ghasia hizi ndiyo za hivi karibuni za ghasia ambayo imekuepo kwa mda wa miezi mingi. Mwaka jana watu 6,000 kutoka kabila la Lou Nuer waliuawa.

Malumbano haya yalianza kama wizi wa mifugo lakini yameongezeka kupita kiasi ambapo mamiya kwa maelfu wamekimbia nyumba zao.

Umoja wa Mataifa pamoja na jeshi la Sudan ya kusini yametuma vikosi zaidi katika mji wa Pabor, ulioshambuliwa siku ya jumamosi ingawa pamoja na nyongeza

ya vikosi bado wamezidiwa kwa idadi ya wapiganaji huku wasiwasi ukitanda juu ya jinsi ya kukabiliana na ghasia hizi bila kuepuka lawama za kuegemea upande mmoja.

Ghasia zimechochewa na wanasiasa. Mwandishi wa BBC wa Afrika mashariki anasema kua ni vigumu kupata picha halisi juu ya ukweli wa mambo katika jimbo la Jonglei ambako taarifa nyingi za mauwaji zimetoka.

Bw.Boloch, kutoka kabila la Murle, amesema kua wakimbizi waliokimbia balaa huko Pibor walifuatwa na kuuawa karibu na mto Kengen, kusini mashariki mwa PiBOR.

Amewashutumu Wanasiasa wa huko kwa kuchochea uhasama uliokuepo kwa miaka mingi kwa manufaa yao binafsi. Ameongezea kua wanaoshiriki mauwaji hayo wengi ni vijana wadogo kabisa.