Polisi Kenya wanasa vilipuzi

Majeshi ya Kenya Haki miliki ya picha internet
Image caption Majeshi ya Kenya

Maafisa wa polisi nchini Kenya wamepata shehena kubwa ya vilipuzi katika kambi ya wakimbizi ya Ifo, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Mkuu wa wilaya hiyo James Ole Siriani amesema washukiwa wawili wanazuiliwa na polisi kusaidia katika uchunguzi zaidi.

Miongoni mwa washukiwa hao ni mke wa mtu anayeaminika kutegeneza vilipuzi hivyo.

Polisi wanasema kukamatwa kwa vilipuzi hivyo ni hatua kubwa katika kuwatambua washukiwa wa visa kadhaa vya mashambulio katika eneo hilo.

Takriban watu 30 wakiwemo maafisa wa polisi wameuawa katika mashambulio ya hivi karibuni katika miji ya Wajir, Mandera na Garissa.

Mashambulio hayo yamekuwa yakiendelea tangu jeshi la Kenya liingie nchini Somalia kuwasaka wapiganaji wa Al Shabaab mwaka jana.

Takriban wakimbizi kutoka Somalia wapatoa nusu millioni wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Dadaad, kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.