Omar al-Bashir azuru Libya

Rais Omar al-Bashir wa Sudan - ambaye anasakwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa kwa mauaji ya watu wengi - yuko nchini Libya kwa ziara ya siku mbili.

Haki miliki ya picha AP

Mashirika ya kupigania haki za kibinaadamu yameeleza malalamiko yao.

Shirika la Human Rights Watch limesema, baada ya kuvumilia kwa miongo kadha uongozi wa kikatili wa Kanali Gaddafi, inatia wasiwasi kuwa serikali mpya mjini Tripoli inazungumza na kiongozi mwengine anayetuhumiwa mauaji vitani.

Sudan imesema iliwapatia silaha wapiganaji waliompindua Kanali Gaddafi mwaka jana.

Uhusiano wa Gaddafi na Sudan ulikuwa mbaya kwa sababu Gaddafi akiwasaidia wapiganaji wa Darfur.