Syria yatakiwa iache kutumia nguvu

Imebadilishwa: 8 Januari, 2012 - Saa 10:38 GMT
Ujumbe wa nchi za Kiarabu, waliovaa makoti ya njano, wamezungukwa na waandamanaji  nchini Syria

Jumuia ya nchi za Kiarabu imetoa wito kwa serikali ya Syria na makundi yenye silaha yaache haraka kutumia nguvu dhidi ya raia.

Mawaziri wa mashauri ya nchi za nje wakikutana mjini Cairo, wameamua kuwa ujumbe walioutuma Syria kuchunguza hali, uendelee na kazi yake, ingawa wapinzani wamelalamika kuwa hausaidii kumaliza fujo huko.

Mawaziri hao walielezewa ripoti ndefu kutoka kwa kiongozi wa ujumbe wao nchini Syria, na wameoneshwa ramani, michoro na picha kuhusu yale wachunguzi walioshuhudia.

Mawaziri hao hawakutaja pendekezo kwamba ujumbe wao uongezwe nguvu kwa kuwajumuisha wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa jumuia hiyo amesisitiza kuwa idadi ya watu waliouwawa imepungua kwa ujumbe wao kuweko nchini Syria.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.