Nigeria yafanya juhudi kumaliza mgomo

Serikali ya Nigeria inakutana na viongozi wa wafanyakazi katika juhudi nyengine za kumaliza mgomo wa juma zima, wa kutaka serikali irejeshe fidia ya bei ya mafuta.

Hapo awali wafanyakazi walikataa pendekezo la serikali la kurejesha nusu tu ya fidia hiyo.

Wafanyakazi wanataka bei ya mafuta irudi kuwa kama ilivyokuwa kabla ya fidia hiyo kuondoshwa wiki mbili zilizopita, na kupelekea bei ya mafuta kupanda mara dufu.

Wafanyakazi kwenye visima vya mafuta wamesema watajiunga na mgomo wa taifa, iwapo makubaliiano hayakufikiwa Jumapili.

Mgomo huo umeugharimu uchumi wa Nigeria mamilioni ya dola, na watu kadha wamekufa katika mapambano na polisi.