Ndege mbili zashambulia Jilib, Somalia

Ndege mbili zimeshambulia mji wa Jilib, kusini mwa Somalia - eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa Kiislamu, la al-Shabaab.

Haki miliki ya picha AFP

Wazee wa mji huo wameiambia BBC, kwamba watoto 6 waliuwawa katika shambulio hilo.

Kuna taarifa zisemazo kuwa wapiganaji wa al-Shabaab ni kati ya watu waliokufa.

Msemaji wa jeshi la Kenya, ameiambia BBC, kwamba alikuwa anajaribu kuthibitisha ikiwa ndege za Kenya zilishiriki katika mashambulio hayo.