Ban Ki-Moon amwambia Assad aache kuuwa

Imebadilishwa: 15 Januari, 2012 - Saa 16:11 GMT

Rais wa Syria, Bashar al Assad, ametoa msamaha wa jumla kwa wale wote waliotenda uhalifu dhidi ya utawala wake tangu kuanza kwa maandamano ya kumpinga mwaka uliopita.

Ban Ki-Moon akizungumza kwenye mkutano mjini Beirut

Wachambuzi wanasema kuwa hatua hiyo inaonekana kuwa jaribio jengine la kutuliza maadnamano hayo.

Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amerudia tena kwa ukali wito wake kuwa Rais Assad wa Syria aache kuuwa watu wake.

Akizungumza katika nchi ya jirani na Syria, Libnan, katika mkutano kuhusu demokrasi katika nchi za Kiarabu, Bwana Ban alisema mapinduzi ya Arabuni yanaonesha kuwa watu hawataki tena kukubali utawala wa kiimla:

"Leo nasema tena kwa Rais Assad wa Syria: acha utumiaji nguvu!

Wacha kuuwa watu wako mwenyewe!

Njia unayopita ya ukandamizaji, haifiki pahala.

Funzo la mwaka uliopita ni wazi kabisa: kwamba mabadiliko yataendelea kutokea.

Mwenge uliowashwa Tunisia hautazimika."

Akizungumza juu ya Israil, Bwana Ban alikariri kuwa ujenzi wa makaazi kinyume cha sheria katika ardhi ya Wapalestina, unaofanywa na Israil, lazima usimamishwe, kwa sababu unazuwia kuanzishwa kwa taifa la WaPalestina litaloweza kujitegemea.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.