Dawa bandia za malaria zaongeza madhara

mgonjwa wa malaria Haki miliki ya picha AFP
Image caption mgonjwa wa malaria

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wamesema kuwa ongezeko la dawa bandia barani Afrika, ni pigo kubwa katika juhudi zinazoendelea za kupambana na maradhi ya Malaria.

Malaria huwaua karibu watu milioni moja kila mwaka katika bara la Afrika.

Wanasayansi wa chuo hicho wamesema kuwa kuuzwa kwa dawa hizo bandia huwadhuru wagonjwa mbali mbali na kusababisha wagonjwa hao kutoweza kupata tiba kamilifu wanapotumia dawa sahihi.

''dawa bandia zatoka Uchina''

Wataalamu hao wa dawa walisema baadhi ya dawa hizo bandia zinatoka Uchina.

Wameshauri kuwa wataalamu wa maswala ya afya katika bara la Afrika wanapaswa kuchukua hatua kambambe za kusitisha kuenea kwa dawa hizo bandia katika bara la Afrika au sio mamilioni ya watu watafariki.

Watu walio taabani sana kutokana na dawa hizo bandia ni watoto na wanawake waja wazito.