Maafisa wavamia wakala wa mafuta Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maandamanno Nigeria, Maafisa wa kupambana na rushwa wavamia ofisi za udhibiti wa bei za mafuta

Maafisa wa kupambana na rushwa nchini Nigerian wamevamia ofisi za wakala wa kudhibiti mauzo ya mafuta huku watu warejea kazini baada ya kumaliza mgomo wa wiki nzima kutokana na kupanda kwa bei za petrol.

Tume ya makosa ya Kiuchumi na Kifedha imesema vifaa vimechukuliwa ili kukaguliwa kutokana na tuhuma za ufisadi kwenye uingizaji wa mafuta unapoanzia.

Nigeira ni nchi inayoongoza kwa utaoaji wa mafuta barani frika lakini inaagiza mafuta yaliyosafishwa kutoka nje.

Mgomo uliitishwa baada ya ruzuku ya gharama za mafuta kuondolewa.

Serikali inasema ruzuku inagharimu $8bn (£5.2bn) kwa mwaka na kwamba fedha hizo zitatumika vema zaidi katika miundombinu na huduma za jamii. Wamiliki wa makampuni yanayoagiza mafuta nchini humo ndio wanufaikaji wakubwa wa ruzuku hiyo na baadhi yao ni matajiri wakubwa nchini humo.

Lakini serikali imepunguza kiwango cha ruzuku hiyo baada ya mgomo na kukubali kurejesha sehemu ya ruzuku hiyo.

Ingawa muungano wa wafanyakazi umeitikia kwa kusitisha mgomo, baadhi ya asasi za kraia zimewataka watu kuendelea na mgomo.

Msemaji wa EFCC Wilson Uwujaren ameiambia BBC kuwa ofisi za wakala wa bei na bidhaa za mafuta-Petroleum Products Pricing Regulatory Agency (PPPRA) mjini Lagos na mji mkuu Abuja, zimevamiwa.

Taarifa za magazeti mbalimbali ya Nigeria zilisema kuwa kampuni ya mafuta ya serikali - Nigerian National Petroleum Corporation – itakuwa chini ya uchunguzi wa EFCC.

Jumatatu serikali ilipitisha kupunguzwa kwa bei ya mafuta ya petrol hadi 97 naira (karibu $0.60) kwa lita na kurejesha sehemu ya ruzuku ya mafuta.

Bei ya petrol ilipanda kutoka 65 naira ($0.40; £0.26) mpaka 145 naira wakati ruzuku ilipoondolewa bila taarifa.

Maandamano hayo yalisababisha vifo vya watu kadhaa katika mji wa kibiashara wa Lagos.