Ravalomanana hakuweza kuingia Madagascar

Ndege iliyombeba rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana, kutoka uhamishoni Afrika Kusini, imelazimishwa kurudi ilikotoka.

Haki miliki ya picha AFP

Msemaji wake alisema wakuu wa safari za ndege Madagascar, yaliamrisha ndege igeuze njia kurudi Afrika Kusini.

Bwana Ravalomanana ameishi uhamshoni tangu mwaka wa 2009, alipotolewa madarakani na Andry Rajoelina.

Tangu wakati huo, juhudi za kupatia ufumbuzi mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo hazikufanikiwa.

Hii ni mara ya pili kwa rais huyo wa zamani kujaribu kurudi nyumbani.