Rais Saleh wa Yemen apata kinga

Imebadilishwa: 21 Januari, 2012 - Saa 16:44 GMT

Bunge la Yemen limekubali kumpa hifadhi Rais Ali Abdullah Saleh ya kutofanyiwa mashtaka.

Maandamano dhidi ya Rais Saleh

Rais Saleh hivi karibuni alitia saini mkataba wa kuondoka rasmi mwezi ujao.

Idhini ya kumpa kinga Rais Saleh ndio ilikuwa kitu muhimu katika makubaliano ya kumfanya rais huyo aondoke madarakani - makubaliano yaliyofikiwa baada ya majirani wa Yemen katika Ghuba, kuingilia kati.

Rais alitia saini baada ya kusitasita mara nyingi.

Na hatimae alipotia saini, bado hapakuwa na hakika kuwa atauheshimu mkataba.

Swala muhimu lilikuwa kuhusu wasaidizi wake wakubwa pamoja na familia yake - ikiwa nao piya watakuwa na kinga.

Sheria iliyopitishwa na bunge la Yemen inawapa kinga ya kadiri fulani, lakini siyo kamili.

Hata hivo hatua hiyo ya bunge itawakera zaidi malaki ya wapinzani wa Rais Saleh, ambao wameendelea kuandamana mabara-barani kudai kuwa kiongozi huyo afikishwe mahakamani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.