Ujumbe wa Kiarabu utabaki Syria

Mawaziri wa nchi za nje wa Umoja wa Nchi za Kiarabu wanaokutana mjini Cairo, wameamua kuzidisha muda wa safari ya ujumbe wao nchini Syria, kwa mwezi mmoja zaidi.

Haki miliki ya picha AP

Wakuu nchini Misri wanasema na maafisa katika ujumbe huo piya wataongezwa.

Umoja wa nchi za Kiarabu unataka kuzidi kuwachagiza wakuu wa Syria waache kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Ujumbe huo umelaumiwa sana na wanaharakati, ambao wanasema kwamba ujumbe huo umetumiwa na Syria, na haukufanya kitu kuzuwia mauaji.

Mwandishi wa BBC wa Mashariki ya Kati, anasema, haikuelekea kwamba kuna mpango mwengine wa kufuata, na hadi sasa hakuna hamu ya kuchukua hatua kali zaidi.