Gingrich apendeza South Carolina

Newt Gingrich amemshinda mpinzani wake mkuu, Mitt Romney, kwenye jimbo la South Carolina, katika kura ya kuchagua mgombea urais wa Marekani, atayewakilisha chama cha Republican.

Haki miliki ya picha Reuters

Bwana Gingrich sasa anaonekana kuwa kiongozi wa mrengo wa kulia wa chama, lakini alishindwa kabla katika majimbo mengine mawili.

Akihutubia wafuasi wake, Bwana Gingrich alisema akichaguliwa kuwa rais, ataunda nafasi za kazi, tofauti na Rais Obama:

"Nataka kupita kila mtaa wa kila kabila, katika sehemu zote za nchi, na kuwaambia watu wazi - ikiwa unataka watoto wako kuwa na maisha ya kutegemea ruzuku ya chakula kwa serikali, basi mgombea wako ni Barack Obama; lakini ukiwa unataka watoto wako wajitegemee wenyewe, basi mgombea wako ni Newt Gingrich, na nina hakika tutapata kura kila pahala."