Maombi maalum kulaani Boko Haram

Haki miliki ya picha INTERNET
Image caption Maombi maalum mjini Kano baada ya mashabulizi ya Boko Haram

wafuasi wa dini ya kiislamu na wakristo wanaoishi Kano,kaskazini mwa Nigeria eneo ambamo zaidi ya watu mia moja na sitini waliuwa wameombwa kutilia maanani siku ya maombi.

kikao cha maombi maalum kimefanyika karibu na Makao Makuu ya Kadhi Mkuu wa Kano ili kumuomba Allah asaidie kusitisha mapigano.

Kundi la kiislamu la Boko Haram limekiri kuutekeleza uvamizi huo, polisi wamesema kuwa zaidi ya vilipuzi kumi na viwili vimepatikana katika magari yaliachwa mjini humo.

Madaktari wamesema kuwa idadi ya watu waliowawa katika misururu ya ulipuaji na ufyatulianaji wa risasi inatarajiwa kuongezeka kwani maiti zaidi zinaendelea kupokelewa katika majumba ya kuhifadhia maiti.

Mwandishi wa BBC mjini humo,Abdullahi Kaura Abubaker, amesema kuwa baadhi ya watu mjini humo wameanza kuingilia shughuli zao za kawaida lakini ulinzi mkali unaendelezwa huko kwingine kukiwa na amri ya kutotembea usiku.

Ombi hilo la kufanya maombi ya pamoja lilitolewa na serikali ya jimbo la Kano pamoja na baraza la ma-Amir katika kituo cha utangazaji cha radio mjini humo.

Waislamu na wakristu waliombwa kukusanyika katika maeneo yao ya kuabudu.

mwandishi wetu wa BBC amesema kuwa takriban watu mia mbili walihudhuria maombi hayo katika msikiti uliopo kati kati mwa Kano huko misikiti mingine mjini humo ikiandaa maombi kama hayo.

Mji wa kano una idadi kubwa ya waislamu hasa eneo la kaskazini, aidha kunao baadhi ya jamii za kikristu.

kundi hilo la Boko Haram lilivamia makundi ya wakristu wakati wa siku kuu ya krismas mwaka uliopita.wakristu ambao ni robo moja ya wakazi wa sehemu ya kaskazini mwa Kano wamehimizwa kuhamia eneo la kusini.

Mamia ya watu wametoroka makwao huku kukiripotiwa kuwepo kwa jamii mbili zinazosaidiana.

Rais wa Nigeria, goodluck Jonathan alizuru eneo hilo kutoa rambirambi zake na kuapa kuyafyeka makundi ya magaidi nchini humo