Rais Goodluck: Boko Haram jitambulisheni

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Goodluck ataka Boko Harama wajitokeze

Rais wa Nigeria ameliambia kundi la kiislamu la Boko Haram wajitambulishe na watoe matakwa yao ikiwa wanataka kufanya gumzo na serikali.

Rais Goodluck Jonathan amesema kuwa hakuna tashwishi kwamba kundi hilo lina uhusiano na makundi ya wanamgambo ya Kiislamu yalio njee ya Nigeria.

Rais huyo amesema ikiwa hawatajitambulisha basi hakuwezi kufanyika majadaliano yeyote na kundi hilo.

Tamko hilo la Goodluck linakuja baada ya kiongozi wa Boko Haram kukanusha kuwa hawakuhusika na mashambilizi ya hivi karibuni katika mji wa Kano uliosababisha vifo vya waru 185.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters Goodluck Jonathan alisema," ikiwa watajitambulisha wazi wazi halafu wasema hii ndio sababu inayotufanya tusababishe vurugu, hii ndio sababu inayotfanya tukabiliane na serikali au hii ndio sababu inayotufanya tuwamalize watu wasiokuwa na hatia yeyote , basi kwanini tusijadiliane?

"Hebu angalia , ukiwa ni Rais wa nchi huwezi kuongoza maiti. Utakuwa rais wa watu waliohai. Kwa hiyo watajitambulisha vizuri basi kutakuwa na msingi wa kufanya gumzo nao"

Alisema anafahamu wasiwasi wa shirika la Umoja wa Mataifa kwamba kundi hilo la Boko Haram linapata mafunzo na silaha kutoka kwa makundi ya kigaidi yaliona uhusiano na al-qaida pamja na Al shabaab.

Na katika Mji wa Kano , viongozi wa Kikristo wameunga mkono tamko hilo la Rais Goodluck Jonathan kama njia ya kumaliza hali ya usalamma inayozidi kuzorota nchini Nigeria.

Kundi lenyewe la Boko Haram limekiri kuhusika na mashambulizi ya vituo vya polisi na majengo mengine ya kiserikali.

Lakini katika ujumbe uliotumwa mtandao wa YouTube, Abubakar Shekau amewalamumu polisi wa Nigeria kwa kuuwa raia wasiokuwa na hatia na pia kuhusika na kuzorota kwa usalama .

Hata hivyo wakuu wa serikali wamekanusha madai hayo.

Wiki iliyopita mji mkuu wapili kwa ukubwa wa Nigeria ulishambuliwa vibaya na Boko Haram na kusababisha vifo vya watu 185 .