Kauli kali kutoka Iran na Israili

Kumekuepo na kauli mpya na kali kutoka kwa viongozi wa Iran na Israel, pamoja na matamshi yaliyoarifiwa kutoka Marekani ikiwa ni kutoka kwa Waziri wa Marekani wa Ulinzi, Leon Panetta - ambayo yanachochea wasiwasi juu ya uwezekano wa malumbano kuhusu mpango wa Iran wa Nuclear.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ayatollah Ali Khamenei

Mataifa ya magharibi pamoja na Israel yanaishuku Iran kua inajaribu kuunda silaha za Nuclea, madai ambayo Iran inakanusha.

Malumbano haya bila shaka yamekua ni kichochezi baridi, ambacho mara kwa mara kimekua kikilipuka. Mlipuko wa sasa ni bayana unaweza kulipuka kwa kiasi kikubwa, kwa matamshi na shinikizo kutoka pande zote.

Sababu moja ni kwamba kuna hisia kua mda unakwenda kuhusiana na shughuli za Iran na uwezo wake wa kuzihifadhi katika handaki.

Pamoja na kutathmini mpango maalum wa Iran na jinsi gani ya kuangalia maonyo inayoyatoa mataifa yaliyo nje yamebaki kuzidisha hofu na mashaka juu ya madai ya Israili.

Kwa kutegemea ripoti mpya ya shirika linalosimamia masuala ya Nuclear la Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi wanachama wa Muungano wa Ulayazimeiwekea Iran vikwazo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta

Lengo likiwa ni kushinikiza tabia za Israel na Iran. Na je hali hii ya sasa kwa pande zote ina ukweli gani? Je Israel inajaribu kupima uwezekano wa kuishambulia Iran, na shambuulio kama hilo litaifaidi nini na athari zake ikiwa Iran itajibu zitakua kiasi gani?

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta anasema kua Marekani tayari imeonyresha wasiwasi wake juu ya uwezekano wa shambulio la Israel.

Hata hivyo Waziri huyo alikataa kutoa jawabu kuhusu taarifa za shambulio kama hilo kutokea katika miezi michache ijayo.