Wanawake wa Saudi wataka endesha gari

Kampeni mpya inaanzishwa nchini Saudi Arabia kuwahimiza wanawake wachukue hatua za kisheria kupinga amri inayowakataza kuendesha magari.

Mwanamke aliyeongoza juhudi za kutaka amri hiyo ibadilishwe, Manal Al Sharif, ameiambia BBC, kwamba atatokeza kwenye kipindi maarufu cha televisheni hii leo, kutangaza hayo.

Anasema ataeleza vipi wanawake wanaweza kufuata mfano wake, kuchukua hatua kisheria, baada ya ombi lake la leseni ya kuendesha gari kukataliwa.

Katika hatua isiyopata kuonekana Saudi Arabia, Bibi Al Sharif ameishtaki serikali - mashtaka ambayo sasa yanazingatiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.