Urusi na Uchina zabeba jukumu la Syria

Imebadilishwa: 5 Februari, 2012 - Saa 14:13 GMT

Mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani kutoka Yemen, Tawakul Karman, amesema Urusi na Uchina zinabeba jukumu la mauaji yanayotokea Syria, baada ya mataifa hayo kupinga kwa kura ya turufu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana.

Tawakul Karman, kulia

Bi Karman piya aliunga mkono wito uliotolewa na Tunisia kuwa nchi zote za Kiarabu zifuate mfano wa Tunisia, na ziwafukuze mabalozi wa Syria.

Chama kikuu cha upinzani cha Syria, SNC, kimelaani kura za turufu za Urusi na Uchina katika Baraza la Usalama kwamba zimeipa serikali ya Syria idhini ya kuuwa.

Shirika la habari la taifa la Syria limeunga mkono msimamo wa nchi mbili hizo na kusema utayapa shime mabadiliko ya kisiasa yaliyoahidiwa na serikali.

Na wapiganaji katika mji wa Homs wanasema vifaru vya jeshi vimekuwa vikiwekwa karibu na mitaa inayodhibitiwa na upinzani.

Mwandishi wa BBC mjini Homs anasema ameelezewa kuwa maiti zimefukuliwa kutoka vifusi vya majengo yaliyoangamizwa kwa mizinga Ijumaa usiku.

Serikali ya Syria imesema taarifa kuwa ilifanya uvamizi mkubwa mjini humo ni uzushi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.