Ugiriki yakubali kukata zaidi bajeti

Maelfu ya watu wameandamana katika miji ya Ugiriki ya Athens na Thessaloniki katika siku ya pili ya mgomo wa saa 48, kupinga hatua kali za kiuchumi za serikali.

Haki miliki ya picha AFP

Polisi wengi wako zamu na usafiri umesimama.

Baraza la mawaziri la Ugiriki limekubali hatua za kupunguza bajeti zaidi, kama yalivoagiza mataifa mengine yananayotumia sarafu ya Euro, ili kuweza kuisaidia Ugiriki kwa dola bilioni kadha, kulipa madeni yake.

Hatua hizo sasa lazima zipate idhini ya bunge la Ugiriki.