Noti mpya za Mandela

Afrika Kusini inatoa noti mpya zenye picha ya Nelson Mandela.

Haki miliki ya picha AP

Rais Jacob Zuma alitangaza hayo mjini Johannesburg katika kutimiza miaka 22 tangu Bwana Mandela kuachiliwa huru baada ya kifungo kirefu.

Alisema kufunguliwa kwa Bwana Mandela ndio ulikuwa mwanzo wa awamu mpya ya matumaini nchini Afrika Kusini.