UN yapitisha azimio kuhusu Syria

Imebadilishwa: 17 Februari, 2012 - Saa 02:34 GMT

Baraza kuu la Umoja wa mataifa limeidhinisha kura ya azimio kuhusu Syria sawa na ile iliyopigiwa kura ya turufu na Urusi na Uchina katika baraza la usalama la umoja huo.

jeshi la syria

Harakati za jeshi la Syria za laaniwa

Zaidi ya theluthi mbili ya wanachama wa baraza kuu la umoja wa mataifa waliunga mkona azimio hilo.

Azimio hilo linalaani mashambulizi yanayotekelezwa na serikali ya Syria dhidi ya wapinzani wake.

Linaunga mkono mpango uliopendekezwa na juimuiya ya nchi ya kiarabu kuhusu mageuzi ya kisiasa nchini humo, ambapo Rais Bashar al Assad ataondoka mamlakani.

Azimio hilo halinatofauti sana na lile ya baraza la usalama la umoja huo ambalo lilipingwa na Urusi na china.

Na kama ilivyo tarajiwa nchi hizo mbili zilipiga kura kupinga azimio hilo.

Hata hivyo waliopendekeza azimio hilo sasa watajigamba kuwa wamepata kuungwa mkono na sehemu kubwa ya wanachama wa umoja wa mataifa.

Urusi ilipinga azimio hilo kuwa halijasisitiza kuwa pande zote mbili hasimu lazima zisitishe mashambulio na pia kuwa mazungumzo yoyote kuhusu mustakabal wa kisiasa wa Syria lazima yahusishe utawala wa sasa.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa halina nguvu za kisheria kushinikiza utekelezwaji wa azimio hilo kwa hivyo matokeo haya hayana uzito sana ila tu kuongeza shinikizo kwa serikali ya syria ikomeshe ghasia zinazo endelea.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.