Watoto Asia wako mbele zaidi kimasomo

Watoto wa shule nchini Pakistan
Image caption Watoto wa shule nchini Pakistan

Watoto wa shule katika maeneo ya Asia wako mbele kimasomo kwa miaka mitatu wakilinganishwa na wenzao katika nchi za magharibi.

Haya ni matokeo ya ripoti mpya ya watafiti nchini Australia, ambao pia wanasema viwango vya juu vya ufaulu havitokani na wazazi kuwashinikiza watoto wao kimasomo au kutumia fedha zaidi kuwasomesha na hitimisho lake ni kuwa na athari za ndani katika maendeleo ya kiuchumi.

Ripoti inasema wastani wa mtoto mwenye umri wa miaka kumi na mitano katika somo la Hisabati Shanghai, Uchina, yuko mbele miaka miwili au mitatu akilinganishwa na mwanafunzi mwenzake nchini Marekani na Ulaya, ambapo wale walioko Korea Kusini wako mwaka mmoja zaidi mbele katika kusoma.

Utafiti huo uliofanywa na Taasisi huru ya Grattan, unasemaAsia Mashariki kwa sasa ni wa nne kwa kuwa na mifumo bora ya shule duniani.

Ripoti hiyo inahitimisha kuwa mtazamo mzuri unalenga katika kile inachokiita mkazo katika masomo, kujifunza kwa vitendo na kuimarisha mafunzo kwa walimu, sio tu kwa kuwa na bajeti kubwa katika elimu.

Ripoti hiyo pia imepuuza umuhimu wa wazazi katika kuwasukuma watoto kimasomo na kuwa na madarasa yenye wanafunzi wachache.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa Shanghai, imeongeza idadi ya watoto katika darasa kufikia 40, lakini wanawapatia walimu muda zaidi wa kupanga masomo.