Mpinzani wa Mutharika augua moyo

Mkosoaji mkubwa wa Rais Bingu wa Mutharika, wa Malawi, Ralph Kasambara, amepelekwa hospitali kutoka gerezani, baada ya kupata ugonjwa wa moyo.

Haki miliki ya picha Getty

Kasambara, ambaye ni mkuu wa sheria wa zamani wa Malawi, alikamatwa kutokana na shutuma za kuhusika na kuwapiga washukiwa watatu, ambao walijaribu kushambulia ofisi yake kwa bomu.

Watu hao watatu walikamatwa na walinzi wa Bwana Kasambara.

Mahakama nchini humo yaliamuru kuwa Bwana Kasambara aachiliwe huru, lakini gereza limekataa kumfungua.

Inaarifiwa kuwa Bwana Kasambara ana azma ya kuanzisha chama kitachompinga rais kwenye uchaguzi wa mwaka 2014.