Aliyenyeshewa theluji aijua

Polisi wa kusini mwa Sweden wanasema wamemuokoa mtu aliyekuwa ndani ya gari iliyofunikwa na theluji, na aliyekuwamo humo bila ya chakula kwa miezi miwili.

Haki miliki ya picha AFP

Maafisa wanasema mwanamume huyo alikutikana amejikunyata kwenye mfarishi wa kulalia, baada ya paa la gari lake kuchomoza na kuonekana kwenye bara-bara inayopita msituni, karibu na mji wa Umeaa, kusini kidogo ya eneo la Arctic.

Mtu huyo kakutikana karibu hawezi kutembea wala kusema na aliwaelezea polisi kwamba hakula tangu mwezi wa Disemba.

Baridi katika eneo hilo hivi karibuni ilishuka na kufika hasi nyuzi 30 centigrade.