Wala kobe watafukuzwa Zimbabwe

Raia wane wa Uchina wanakabili amri ya kufukuzwa Zimbabwe, baada ya kukamatwa kwa sababu waliwauwa na kuwala kobe adimu.

Haki miliki ya picha

Wakuu wanaohusika na wanyama, wanasema Wachina hao wamekiri mashtaka ya kuwafanyia ukatili wanyama hao.

Wachunguzi wanasema walikuta magamba ya kobe 40, aina ya Bell's Hinge - aina adimu ya kobe.

Piya walipoingia ndani ya nyumba ya wanaume hao wa Kichina, walikuta kobe wengine 13 kwenye mapipa, wamewekwa bila ya kupewa maji au chakula.

Kobe hao hutumbukizwa ndani ya maji yanayochemka, wakiwa hai.