Sahel yahitaji msaada zaidi

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa baada ya ombi lake la msaada kwa ajili ya Niger, umepata asili-mia-10 tu ya lengo lake, huku ukame na njaa inaendelea kuathiri watu milioni-12 katika kanda yote ya Sahel.

Akizungumza mjini Agadez, kasjkazini mwa Niger, Helen Clark, wa shirika moja la msaada la Umoja wa Mataifa, aliiambia BBC kwamba ameona watoto wanatapia mlo vibaya na akina mama dhaifu sana.

Umoja wa Mataifa umeomba dola 700-milioni kuweza kukidhi mahitaji ya eneo hilo.

Nchi kadha, kutoka Mauritania hadi Chad zimekumbwa na ukame, na watu wengi wanahama vijiji vyao, kutafuta msaada mijini.