Vikwazo vyaiumiza Syria

Mfanya biashara mmoja maarufu wa Syria anasema uchumi wa nchi hiyo unaumia kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi vilivowekwa na nchi nyengine dhidi ya Syria na kwamba Rais Bashar al-Assad na serikali yake haikuelekea kuweza kudumu zaidi ya miezi sita.

Haki miliki ya picha AFP

Faisal al-Qudsi, mtoto wa rais wa zamani wa Syria, aliiambia BBC kwamba vikwazo dhidi ya mafuta ya Syria na utalii kupotea, kumepunguza pato la taifa kwa asili-mia-45.

Alisema serikali ya Syria inapata pesa kutoka Iran lakini hazitoshi na wafanya biashara wa Syria wameacha kumuunga mkono Rais Assad.

Alisema wafanya biashara wengi wanahofia maisha yao na wameondoka nchini.