Uchumi wa Ugiriki kuchepuliwa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Beji ya EU yenye bendera ya Ugiriki

Huku mawaziri wa bara Uropa wakikutana mjini Brussels kuamua ikiwa waedelee na mpango mpya wa kuchepua uchumi wa Ugiriki, waziri wa fedha wa Ufaransa Fran├žois Baroin, amesema mikakati yote iko sambamba ikiubiriwa tu makubaliano.

Waziri mwenzake wa Ugiriki, Evangelos Venizelos, amesema kuwa anatarajia kipindi kirefu cha sintofahamu kuhusu uchumi wa Ugiriki kukamilika leo.

Makubaliano hayo yataiwezesha Ugiriki kupokea mikopo ya zaidi ya dola bilioni miamoja sabini huku madeni yake yaklifikia mabilioni ya dola yakifutwa.

Hata hivyo makubaliano hayo yamekubwa na utata kuhusu namna ya kuhakikisha kuwa Ugiriki itatii masharti kupunguza matumizi ya pesa za umma.