Somalia kupata tiba Mjini London.

Imebadilishwa: 23 Februari, 2012 - Saa 02:04 GMT

Tishio la ugaidi na uharamia ni miongoni mwa maswala yatakayo jadiliwa katika mkutano huo wa London kuhusu hatma ya Somalia.

Wanajeshi wa Amisom wawasili nchini Somalia

Wawakilishi kutoka nchi 40 watahudhuria mkutano huo wenye lengo la kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba nchi hiyo kufuatia miongo miwili ya vita na ukame.

Viongozi wanatarajiwa kukubaliana kuhusu pesa za ujenzi wa shule, hospitali na idara ya polisi.

Uingereza imetaja Somalia kama nchi iliyoporomoka zaidi duniani lakini imesema kuna haja ya kuipa Somalia nafasi nyegine ili iweze kuibuka kutoka matatizo yake.

Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali, ambaye ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria mkutano huo ameonya kuwa nchi yake iko katika njia panda na inahitaji usaidizi mkubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa.

Waziri wa Mambo ya njee wa Marekani Bi Hilary Clinton, Raisa wa Nigerian Goodluck Jonathan, Kiongozi wa Ethiopian Meles Zenawi na katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa , Ban Ki-moon ni miongoni tu mwa viongozi wanaohuduria

Siku ya Jumatano Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kupanuliwa kwa jeshi la Umoja wa Afrika linalohudumu Somalia kutoka 12,000 hadi karibu 18,000.

Baraza hilo la Usalama pia iliongeza muda wa jeshi hilo la Afrika na pia kukubali kuligharimia.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.