Senegal yaombwa itulie

Viongozi wa kimataifa wameisihi Senagal kuwa tulivu kabla ya uchaguzi wa Jumapili, ambapo Rais Abdoulaye Wade anagombea muhula wa tatu wa uongozi.

Haki miliki ya picha AFP

Uamuzi wa kiongozi huyo wa miaka 85, wa kugombea tena urais kinyume na katiba iliyoweka mihula miwili tu, umezusha maandamano ya majuma kadha.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-Moon, ametoa wito wa uchaguzi wa amani na wa kuaminika.

Rais wa sasa wa Umoja wa Afrika - Thomas Boni Yayi wa Benin - amewasihi watu wa Senegal wasahau hitilafu zao.