Waumini wauwawa Nigeria

Mshambuliaji aliyejitolea mhanga amewauwa waumini kama watatu na kuwajeruhi karibu 40 wengine kwenye kanisa katika mji wa Jos, Nigeria.

Kasisi mmoja aliiambia BBC kwamba mlinzi aliyekuwa zamu nje ya kanisa hilo, aliruhusu gari la mshambuliaji kuingia kwenye uwanja wa kanisa, wakati wa ibada ya asubuhi.

Hilo ndilo shambulio la karibuni kabisa katika mfululizo wa mashambulio dhidi ya Wakristo, tangu watu zaidi ya 40 kuuwawa kwenye kanisa, karibu na mji mkuu wa Nigeria, Abuja, siku ya Krismasi.