Syria yafanya kura ya maoni

Kura ya maoni kuhusu katiba mpya inafanywa nchini Syria hii leo, ingawa ghasia zinaendelea nchini.

Haki miliki ya picha Getty

Kura hiyo ni muhimu katika utaratibu wa kuleta mabadiliko yaliyopendekezwa na Rais Bashar al-Assad, ili kujibu maandamano dhidi ya serikali yake yaliyoanza karibu mwaka mzima uliopita.

Katiba mpya itaruhusu mfumo wa vyama vingi nchini Syria.

Upinzani umetoa wito watu waisusie kura hiyo.

Mwandishi wa BBC anasema haijulikani vipi kura ya maoni inaweza kufanywa kati ya mtafaruku ulioko nchini humo.