Wenger Arsenal ' bado ni hai '

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsene Wenger meneja wa Arsenal asema timu yake 'iko hai'

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anasema Arsenal " bado hai " kinyume na wengi walivyofikiria baada ya kuilaza Tottenham Hotspurs kwa mabao matano kwa mawili.

"Jinsi tulivyocheza ilikuwa safi kabisa licha ya kuanza vibaya"aliongeza.

Bao la Louis Saha na mkwaju wa penalti wa Emmanuel Adebayor uliiweka Spurs katika hali ya kufikiria ushindi dhidi ya watani wao wa jadi.

Lakini Bacary Sagna na Robin van Persie walisawazisha kabla ya kipindi cha mapumziko. .

Tomas Rosicky akafunga muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili na mabao mawili ya haraka yaTheo Walcott yaliwakatisha tamaa Spurs na kufufua matumaini ya Arsenal ya kufuzu kucheza katika Ligi ya Ulaya katika msimu ujao.