Meli ya ng'ombe yakatazwa kuingia Misri

Watetea haki za wanyama wameiomba Misri au Djibouti zikubali meli yenye matatizo na iliyosheheni maelfu ya ng'ombe itie nanga bandarini.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Shirika liitwalo "Huruma kwa Wanyama" linasema kuwa limepata taarifa kuwa ng'ombe karibu 3000, kwenye meli iitwayo Gracia del Mar, wameshakufa.

Meli hiyo imetia nanga kwenye Bahari ya Sham, tangu ilipopata matatizo kwenye mitambo na imekataliwa kushusha mali katika nchi iliyokuwa ikielekea, yaani Misri.

Meli hiyo ilianza safari yake Brazil, majuma kadha yaliyopita.

Haijulikani kwanini ilizuwiliwa kuingia bandarini, nchini Misri.