Msalaba Mwekundu wajaribu kufika Homs

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Syria limesema linatarajia kufikisha msaada wa dharura katika mtaa wa Baba Amr mjini Homs leo, baada ya serikali kuzuia msafara wake kuingia humo Ijumaa.

Haki miliki ya picha AFP

Msemaji wa shirika hilo amesema watafanya kila wawezalo kuwafikia waathiriwa.

Mpiga picha wa Uingereza, Paul Conroy, ambaye alikimbizwa kwa siri kutoka mji huo wiki hii, aliiambia BBC kuwa eneo hilo linashuhudia mauwaji ya raia kwa mpango.

Bwana Conroy ambaye alinusurika na shambulio la kombora ambalo liliuwa waandishi wa habari wawili kutoka Ulaya, alisema nia ya jeshi la Syria kuupiga mizinga mtaa wa Baba Amr ni kuwaangamiza wakaazi wa huko.

Alisema wakaazi wanapigwa mizinga kutwa na kila siku, na maisha yao ni kujaribu kuhepa mashambulio hayo.