Depo ya Brazzaville yaripuka

Watu wengi wanaarifiwa kufa katika Jamhuri ya Congo, baada ya mfululizo wa miripuko mikubwa, kwenye kambi ya jeshi, katika mji mkuu, Brazzaville.

Haki miliki ya picha wikipedia brazzaville

Miripuko hiyo ilisababishwa na moto kwenye depot ya silaha.

Taarifa zisizothibitishwa zinaeleza kuwa watu zaidi ya 150 walikufa na mamia kadha kujeruhiwa.

Miripuko hiyo ilibomoa nyumba na kuwafanya wakaazi kuikimbia mitaa ya mashariki mwa Brazzaville.

Piya kishindo kilisikika umbali wa kilomita kadha, katika nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, na kuvunja madirisha mjini Kinshasa.