Chelsea yamfurusha Kocha Villas Boas

Villas Boas Haki miliki ya picha bbc
Image caption Ndoa imevunjika

Habari moto moto kutoka mtandao wa klabu ya Chelsea inayocheza katika Ligi kuu ya England,zasema kua klabu hio imeachana na kocha Andre Villas-Boas leo jumapili.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 34 amepoteza kazi hio saa 24 baada ya kupoteza jana pambano la Ligi dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion 1-0.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Roberto Di Matteo

Kufuatia mechi ya jana Chelsea ilijikuta katika nafasi ya tano kweenye msimamo wa Ligi.

Tangazo la Chelsea limesema kua aliyekua naibu wa Kocha huyo Roberto Di Matteo atashikilia wadhifa wa Kocha hadi mwisho wa msimu.