Iran haiwezi kutengeza silaha za nuklia

Rais wa Israil, Shimon Peres ameuambia mkutano wa Wamarekani wanaoitetea Israil nchini Marekani, kwamba Iran ni hatari kwa ulimwengu mzima.

Haki miliki ya picha AFP

Alisema serikali ya Iran haina maadili na kwamba inagharimia ugaidi duniani na lazima izuwiwe na itazuwiwa.

Alisema Marekani na Israil zina lengo moja kwamba Iran haitaruhusiwa kutengeneza silaha za nuklia.

Na Rais Obama ameonya kuwa Marekani haitasita-sita kutumia nguvu ili kuizuwia Iran isipate silaha za nukliaa - lakini alisema yeye anapendelea kutumia njia za kidiplomasia.

Piya alionya watu kutotumia neno vita kwa urahisi katika mzozo na Iran.

Bwana Obama alikuwa akitoa hotuba muhimu mbele ya kamati ya inayotetea uhusiano mwema baina ya Israil na Marekani.