Wafadhili watokomee asema Mutharika

Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, ameshambulia vikali serikali za kigeni na mashirika yanayojitegemea, yaani NGO: aliyashutumu kuwa yanapanga njama ya kuipindua serikali yake.

Haki miliki ya picha Getty

Akiwahutubia wafuasi, Rais Mutharika alisema amechoka kutukanwa, na wafadhili nao watokomee.

Aliwasihi wafuasi wake kuzuwia maandamano yoyote yale dhidi yake.

Uingereza, Umoja wa Ulaya, na wengineo, pamoja na Benki ya Dunia, zilisimamisha msaada kwa serikali ya Malawi mwaka jana.