Milipuko ya Brazzaville yaua watu 200

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Moshi wafuko toka Brazzaville

Watu wapatao 200 wathibitishwa kuuawa kufuatia milipuko katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Congo ,Brazzaville.

Mishindo mikubwa ilisikika kilomita kadhaa nje ya mpaka wa Congo hadi mjini Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Imearifiwa kuwa mamia ya watu walijeruhiwa kutokana na milipuko hiyo.

Mwandishi wa BBC Patrice Chieta anasema wengi ya wakaazi wa mashariki mwa Brazzavillle walikimbia nyumba zao kufuatia milipuko hiyo.

Anasema milipuko hiyo ilianza majira ya saa mbili asubuhi na ikaendelea hadi mchana.

Wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhi maiti mjini Brazzaville wamesema walihesabu maiti 136 huku maiti zaidi zikiendelea kupokelewa. Na hospitali nyigine zilizo mjini ziliriarifiwa kupokea maiti 70 zaidi.

Akizungumza kupitia Radio ya kitaifa , Waziri wa Ulinzi wa Congo Charles Zacharie Bowao, alisema milipuko hiyo ilisababishwa na moto uliotokea katika ghala la kuhifadhia silaha kwenye kambi ya kijeshi eneo la Mpila.

Na baadae Waziri huyo alionekana katika Runinga ya kitaifa akiwasahuri wa Congo Brazzaville wawe na utulivu.