Wanajeshi Waingereza wauawa Afghanstan

Image caption Mwili wa mmoja wa askari wa Uingereza ukirejeshwa Uingereza, sita wameuawa katika mlipuko

Wanajeshi sita wa Uingereza wameuawa Kusini mwaAfghanistan baada ya gari lao kulipuliwa na kuifanya idadi ya vifo vya wanajeshi wa Uingereza nchini humo kufikia 404.

Wanajeshi hao walikuwa ndani ya gari la deraya katika eneo la Lashkar Gah saa moja usiku wakati gari lao lilipokumbwa na mlipuko mkubwa na wote waliokuwemo ndani ya garihilowaliuawa.

Walikuwa katika eneo lisilo na wakazi wengi.

Hata hivyo wapiganaji wa Taliban wanaendelea kutega mamia ya mabomu katika miji ya Helmand naKandahar.

Hii ndio idadi kubwa zaidi ya vifo vya wanajeshi wa Uingereza katika tukio moja nchiniAfghanistantangu kuanguka kwa ndege ya muundo wa Nimrod mwaka 2006 ambapo wanajeshi 14 waliuwawa.

Idadi ya vifo vya wanajeshi wa Uingereza nchiniAfghanistan imefikia 404 tangu mwaka 2001.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema imekuwa "siku ya msiba mkubwa kwa taifa, inatukumbusha jinsi inavyotugharimu kwa kazi tunayoifanya nchini Afghanistan na mchango wa wanajeshi wetu wanavyoendelea kujitoa mhanga," aliongeza.

"naamini hii ni kazi muhimu kwa usalama wa taifa letu na bila ya shaka kazi hii itakuwa ikitekelezwa na wanajeshi wa Afghanistan na sote tunataka kuona mageuzi haya yanafanyika."