Al Bashir kushtakiwa kwa mauwaji Nuba

Mukesh Kapila Haki miliki ya picha online
Image caption Mukesh Kapila

Aliyekua afisa mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya haki za binadamu kwa ajili ya Sudan ameituhumu serikali ya Sudan ya kaskazini kwa uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo la milima ya Nuba, kwenye mpaka na Sudan ya kusini.

Afisa huyo, Mukesh Kapila, aliyetembelea eneo hilo amesema uhalifu huu wa kuyafyeka makabila ya Wa Nuba, unafanyika dhidi ya baadhi ya wale ambao wamekua wakipigana dhidi ya utawala wa Sudan.

Bw. Kapila ameiambia BBC kua alishuhudia mwenyewe ndege za majeshi ya serikali ya Sudan zikipaa kupitia milima ya Nuba bila kujali kama wanaopigwa ni waasi au ni raia.

''Alisema tulisikia miliyo ya ndege na kuziona zikipaa karibu na tulipokua.

Kisha tukawaona wanawake na watoto, ambao nilizungumza nao mda mfupi kabla ya kutokea kwa ndege hizo walikimbilia katika mapango na myanya iliyo kwenye vilima ambako daima wamezowea kukimbilia kila ndege hizo zinapojitokeza.''

Bw.Kapila alisema kua alichoshuhudia katika milima ya Nuba kilimkumbusha sera ya kuchoma ardhi ambayo ilianzishwa na utawala wa Khartoum katika eneo la Sudan ya magharibi huko Darfur.

"vijiji vilivyochomwa. Tuliona jinsi visima vya maji vikilengwa. Tukaona makanisa yakiteketezwa kwa sababu huenda watu wakakimbilia humo kunusuru maisha yao. Na pia tulishuhudia, kwa mara ya kwanza ripoti ya matumizi ya bomu za ardhini pamoja na mabomu yanayolipuka na kueneza gesi yenye sumu hewani.''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Omar al Bashir

Bw.Kapila amebashiri kua huenda mavuni yatakayoweza kupatikana yakafikia asili mia tano hadi kumi na tano mwaka huu, kutokana na mfululizo wa mabomu yanayodondoshwa huko.

Pamoja na kuikaripia serikali ya Sudan mjini Khartoum, Bw.Kapila ameonekana kuchoshwa na Umoja

"taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hivi karibuni haikuwa na lolote muhimu.

Maelezo yake yasiyo kua na maana yameichagiza serikali ya Khartoum kuzidisha juhudi zake ikifahamu vyema kua ulimwengu hautochukua hatua yoyote.

Serikali ya Sudan imesisitiza kua hatua yake huko Nuba ni kwa lengo la kuwapiga waasi.

Lakini Bw.Kapila amesema kua kuna uwezekano wa kua Bw.Omar Al Bashir ambaye tayari anakabiliwa na tuhuma za visa vya kihalifu huko Darfur, huenda akakabiliwa na mashtaka kama hayo kwa yanayoendelrea katika milima ya Nuba.