Waziri wa Syria ajiondoa serikalini

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Naibu waziri wa mafuta wa Syria, Abdo Husa-meddin

Naibu waziri wa mafuta nchini Syria Abdo Husa-meddin amejiuzulu kutoka serikali ya Rais Bashar Al Assad ili kujiunga na kile alichokiita mapinduzi ya raia wa Syria.

Anakuwa afisa wa ngazi ya juu zaidi kumuasi rais Assad tangu kuanza kwa harakati za mapinduzi yanayoongozwa na raia nchini humo mwaka mmoja uliopita.

Hussam-eddin ambaye ametoa ujumbe huu kupitia tovuti ya YouTube akisema anajiunga na wananchi katika maandamano yao, amesema anatarajia maafisa wa utawala nchini Syria wataweza kujibu hatua yake kwa kuchoma nyumba yake na kusaka familia yake

Amewataka maafisa wengine wa serikali kujiondoa kutoka serikali ya rais Asaad.

Akiwa amevalia, kote na suti , naibu waziri huyo, alisoma ujumbe wake wa dakika nne wa kujiondoa kwenye utawala wa Asaad, akisema kuwa amekuwa kwenye nyadhifa mbali mbalia serikalini kwa miaka thelathini na tatu.

Image caption Ramani ya Syria

Aliongeza kuwa kwa mwaka mmoja uliopita, utawala wa Asaad, umekuwa ukiwakandamiza wananchi kiasi cha kufikisha nchi hiyo katika vita.

Aliwasihi wenzake kujiunga naye akisema kuwa baada ya mwaka mmoja wa kimya kikuu, damu ya waliopoteza maisha yao wakipigania mapinduzi, haitawoondoka mikononi mwao ikiwa wataendelea kufanya uhalifu dhidi ya binadamu kwa kisingizio kuwa wanatii amri ya serikali.

Duru za upinzani ziliarifu kuwa vikwazo kama vya kuteketeza nyumba za wale wanaojizulu kutoka serikali pamoja na kuwasaka familia zao, ndivyo vinatishia maafisa wengi wakuu wa serikali kujiondoa kwenye serikali ya Asaad au hata jeshini.

Kujiuzulu kwa waziri huyo,huenda ni ishara ya mivutano serikalini huku ghasia ikichacha na uchumi ukizorota zaidi kwa sababu ya vikwazo.