Annan akutana tena na Assad

Mjumbe wa kimataifa aliyetumwa Syria, Kofi Annan, anasema wakati wa duru ya pili ya mazungumzo na Rais Bashar al-Assad, amekabidhi mapendekezo thabiti ya kuzimua msukosuko wa sasa.

Haki miliki ya picha AFP

Lakini Bwana Annan alikiri kuwa itakuwa kazi ngumu kufikia makubaliano ya kusitisha umwagaji damu:

"Itakuwa kazi kubwa, itakuwa vigumu, lakini lazima tuwe na tamaa.

Mimi nina matumaini, nina tamaa kwa sababu kadha.

Kwanza nimekuwapo hapa kwa muda mfupi sana; na karibu kila mwananchi wa Syria niliyekutana naye anataka amani.

Wanataka ghasia zimalizike waendelee na maisha yao.

Nimekabidhi mapendekezo thabiti kwa rais, ambayo yakikubaliwa, yataleta mabadiliko.

Yatasaidia kuanzisha utaratibu na kusaidia kuzimua msukosuko."

Siku ya Jumamosi Rais Assad alikataa mazungumzo ya kisiasa wakati wale aliowaita "magaidi" wanafanya shughuli zao nchini.