Maziko makubwa yafanywa Brazzaville

Haki miliki ya picha AFP
Image caption watu wakisaka mabaki katika kanisa la St Louis mjini Brazaville baada ya mlipuko kutokea katika ghala la silaha

Mazishi yamefanywa katika Jamhuri ya Congo, ya watu 200 waliokufa kwenye milipuko iliyotokea kwenye depo ya kambi ya jeshi ya mji mkuu, juma lilopita.

Maelfu ya watu wamehudhuria sala ya wafu mjini Brazzaville.

Haijulikani hasa idadi ya watu waliokufa; wataalamu wa mabomu wanasema inaweza kuchukua miaka, kabla ya eneo lilo karibu na depo kuwa salama kuishi.

Makanisa ya Brazzaville yanawapa hifadhi watu kama 14,000 waliopoteza makaazi kwenye miripuko hiyo.

Muombolezi mmoja aliyepoteza mama ake alisema, makosa yalikuwa ya wakuu, kuruhusu depo hiyo kuwa kati ya mji mkuu.